Updates kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam leo ni kuhusu pia hawa Waalimu pamoja na Mkurugenzi wa Shule ya Awali na Msingi Mount Pleasant Tabata kufikishwa Mahakamani.
Walimu waliofikishwa Mahakamani ni 12 pamoja na Mkurugenzi wao wakikabiliwa na kosa la kuishi Tanzania kinyume na sheria.
Washtakiwa hao ni Anna Ochwo, Josephine Nelson (Mhasibu), Janeth Onzia, Upakmungu Nobert, Abitegeka Israel, Hajara Umavu, Sibibuka Emmanuel na Stedia Chalikunda.
Wengine ni Evelyn Rikoba, Mkamwagi Flavia , Byamugisha Fambe, Margaret Apophia(Meneja) na Julius Nelson (Mkurugenzi).
MFANYABIASHARA WA TANZANIA ALIEHUKUMIWA MIAKA 10 JELA LEO DSM