Mtandao njia mpya kubwa ya mawasiliano kwa kila mtu hivi sasa, World Lung Foundation wameona wasogeze hii huduma kwa kila mtu ambapo itakuwa rahisi tu mtu kuhudumiwa kwa njia ya mtandao.
Huduma hiyo imezinduliwa leo Dar, World Lung Foundation imerahisisha kwa kuisogeza huduma hii ambayo itasaidia kutoa huduma kwa akina mama wajawazito ppamoja na watoto kwa njia ya mtandao.
Tunajua kuna changamoto ya uhaba wa vituo vya huduma za afya, lakini hii njia ya mtandao itasaidia kwa kiasi kikubwa watu kupata msaada hata katika vituo vidogo vya afya.
Mfumo huu wa kutumia mtandao utasaidia wafanyakazi wa vituo vya afya kuongeza uwezo wao wa kutoa huduma katika kliniki za huduma za afya.