January 14, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Mwigullu Nchemba kwa kushirikiana na Wizara nyingine wamefanya ukaguzi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA) ili kubaini changamoto za utendaji kazi wa uwanja huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwigullu amesema idadi ya wageni wa utalii na wanaokuja kuwekeza imeongezeka nchini hivyo watajitahidi kuboresha huduma.
Mwigullu amesema mbali ya kuboresha huduma hiyo, pia wataboresha huduma ya Passport na Visa kutoka kwenye mfumo wa zamani na kuwa wa kisasa wa Kielektroniki.
“Wizara tupo katika hatua ya kuhama kutoka Passport ya kawaida kwenda kwenye Passport ya kimtandao ambapo hadi kwenye Visa, mchakato huo sio wa siku moja Bali tutaongeza na idadi ya watumishi”– Dr. Mwigullu
VIDEO: ALICHOONGEA KIGWANGALLA BAADA YA KUFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE NA DR. MWIGULLU