Siasa na headlines zake kila kukicha, ninayo hii ya jana JUNE O4 2015 Mwanza.. Kama ulipitwa nimeamua kukusogezea hizi sentensi 10 za Mbunge William Mganga Ngeleja akizungumzia sababu ya kusimamisha Uwaziri na ishu ya Urais wa TZ.
“Imekuwa ikisemwa kwamba mimi niliondoshwa Uwaziri kwa kashfa, lakini kumbukumbu zipo na mamlaka zinafahamu.. natumia nafasi hii kuwafahamisha kwamba mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete mwaka 2012 niliondoshwa kwenye Uwaziri.. yalikuwa ni mabadiliko ya kawaida.”
“Mimi sio Waziri wa kwanza kubadilishwa kwenye nafasi ya Uwaziri.. kwenye nafasi ya kuteuliwa mwenye mamlaka ya kukuweka ndio mwenye mamlaka ya kukuondoa.. sikuondoshwa kwa kashfa”
“Urais unaombwa na wengi ndio lakini mimi sio msemaji wa wenzangu.. mimi ninaongozwa na dhamira yangu kupambana na umaskini, maradhi, rushwa, ujinga, ufisadi na mmomonyoko wa maadili.. nimejitokeza kuwaomba Watanzania waniunge mkono.. naamini ninafaa kwenye mazingira ya sasa kuliko yoyote alliyejitokeza“>>> William Mganga Ngeleja.
Sauti yake yote iko hapa, utamsikiliza Mbunge Ngeleja alichokiongea alipokuwa akitangaza nia Mwanza.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.