Polisi katika mji wa Mashariki wa India Bihar wamewakamata wanaume wanne kwa tuhuma za kumwingilia kinyume na maumbile mwanamke mmoja huku wakichukua video za kitendo hicho.
Inaelezwa kuwa baada ya kufanya kitendo hicho, wanaume hao walizituma video hizo kwenye mitandao ya kijamii.
Video hiyo inaonesha wanaume saba wakimshambulia mwanamke mmoja katika eneo la Jahanabad na hadi sasa polisi wanaendelea kuwatafuta wanaume wengine watatu waliobaki.
Inaelezwa kuwa wanaume hao walifanya jambo hilo kwenye eneo la wazi huku mwanamke huyo akiomba msaada, lakini waliokuwa wakiangalia tukio hilo waliendelea kuchukua video bila kutoa msaada wowote.
Kilichosababisha wakina Mama kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Arusha