Ni Julai 28 ,2023 ambapo Mtoto wa Mwigizaji Star Wolper aitwae Paris amepewa ubalozi wa Duka la Nguo za watoto llitwalo Rosly Kids lililopo Sinza Kumekucha Dar es Salaam na akiwakilishwa na Mama yake mzazi wakati wa utambulisho wa ubalozi huo uliofanyika Sinza siku ya leo hii.
Wolper ambaye amefunguka baada ya mtoto wake kupata Dili hilo akisema amekuwa mzito sana kupokea madili ya kazi kwa watoto wake sababu amekua akiangalia ubora wa kampuni au bidhaa husika hivyo hata Duka hilo kumpa ubalozi mtoto Wwake ni baada ya kuridhishwa sana na ubora wa vitu vyao.
Katika mengine mwa kubwa aliyoongea Wolper amezungumzia ishu ya mumewe Rich Mitindo kuwepo China Kwa Muda mrefu ambapo amekiri ni kweli atakaa China Kwa mwaka mzima na amemruhusu kuchepuka ila ajikinge na magonjwa.
“Aendelee kupambana akumbuke Sasa hivi Sio Rich ni Baba P, Ajiheshimu akichepuka atumie kinga, Fanya mambo huko lakini tumia kinga, usichepuke na mtu hauna Faida naye” Wolper