Baadhi ya watu wamekua na Imani tofauti kuhusu kuandika Wosia wa mirathi kwamba unajitabilia kifo jambo ambalo halina ukweli wowote bali inasaidia kuondoa migogro ya kifamilia kwenye mirathi.
Hayo yamebainishwa na Mhe. Jaji Mfawidhi wa Mahakama yabRufanu Mhe. Alvin WA Mugeta wakati wa mdahalo maalum wenye mada ya namna ya usimamizi bora wa mirathi uliofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu ya Morogoro
Mhe. Jaji Muget, ameeleza ni muhimu kwa watu wote kama kuna mali uliochuma kupanga matumizi yake Kwa kuandika Wosia ambao Utakuwa mwarobaini wa migogoro ya kifamilia ambayo imekua ikivunja amani na kuleta uadui
Aidha, ameiomba jamii kuona umuhimu mkubwa wakuacha Wosia, kwa suala hili lisipofanyiwa kazi litaleta athari katika na mwamba wananchi wanatakiwa kupewa elimu juu kuandika kwa kuonesha mpangilio maalum wa Mali wangapi hai.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi HEET Namba 04 unaolenga kuwawezesha vyuo vikuu kuwa wahitimu bora wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira Dkt. Albogast Msabilia amsema kuwa, mradi huu umelenga kutekeleza katika sehemu saba lakini kwa leo unatekeleza katika sehemu ya nne ambacho unaimarisha uhusiano chuo kikuu mzumbe na sekta binafsi pamoja na wadau wengine wakiwemo wananchi na wanafunzi wa sheria chuoni hapo Ili waweze kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Mradi wa HEET ni mradi wa kitaifa umelenga utoaji wa elimu ili wanafunzi waweze kufanya vizuri pia mradi umegawanyika katika sehemu saba na sehemu ya nne unalenga kuboresha uwelewa kile kinachafundishwa kiweze kufanyiwa kazi katika Jamii.