Serikali katika Mji Mkuu wa Korea Kusini inatarajiwa kutambulisha mfumo mpya ambao utalazimisha wafanyakazi kuondoka maeneo yao ya kazi kwa wakati kwa kuzima kompyuta zote ifikapo saa 2:00 usiku siku za Ijumaa.
Imeeleza kuwa jitihada hizo zinalenga kupunguza tabia ya wafanyakazi kuzidisha muda wa kufanya kazi maofisini. Nchi ya Korea Kusini inatajwa kuwa moja kati ya nchi zenye masaa mengi ya kufanya kazi duniani kote.
Inaelezwa kuwa wafanyakazi wa serikali nchini humo wanafanya kazi kwa wastani wa saa 2,739 kwa mwaka, ambayo ni masaa 1,000 zaidi ya kufanya kazi ukilinganisha na nchi zilizoendelea.
Utekelezaji wa jambo hili umepangwa kuanza March 30, 2018, ambapo kompyuta zote zitazimwa ifikapo muda huo uliopangwa.
TBT: Meli ya TITANIC ilivyozama na kuua maelfu ya watu