Serikali ya Israel imetangaza kufutilia mbali mpango wa kuwafukuza kwa lazima kutoka nchini humo maelfu ya wahamiaji haramu kutoka barani Afrika.
Serikali hiyo imeandika barua kwenda katika mahakama ya juu zaidi ya Israel na kueleza kuwa suala la serikali kuwatimua kwa lazima wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika, “sio suala kuu katika ajenda”.
Barua hiyo imeeleza kuwa, maafisa wa uhamiaji wa Israel wanatafuta njia ambayo watawahamisha wahamiaji hao kutoka Afrika kwa hiari.
Ushauri wa Halima Bulembo kwa Wapinzani “hawana hoja”