Nchi mbalimbali duniani zikiwa zinajiandaa kuhudhuria Kongamano la Wafadhili litakalofanyika mjini Geneva nchini Uswisi mwezi ujao Serikari ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa kuhudhuria kongamano hilo.
Imeeleza sababu za kutohudhuria kongamano hilo kuwa nchini yao imekuwa ikitangazwa vibaya ulimwenguni.
Umoja wa Mataifa umeeleza lengo kuu la kongamano hilo ni kuchangisha kiasi cha fedha takribani Dola za Marekani Bilioni 1.7 sawa na Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.08 ili kusaidia wenye mahitaji mbalimbali nchini humo.
Ripoti zinaonesha kuwa watu takribani Milioni 13 nchini DRC wanahitaji misaada, Milioni 4.5 kati yao hawana makazi maalumu huku wengi wakiathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Sababu zimetajwa za Vyuo Vikuu kufungiwa nchini
Mama Ashura ndio sababu ya ukimya wa Ebitoke na Bwana Mjeshi? Wazungumza hapa