Kama kawaida Ayo TV na millardayo.com hukuletea story kazi za ndani pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania. Na leo ni kuhusu Tsunami ya Tohuku iliyotokea mwaka 2011 huko nchini Japan.
Ilikuwa March 11, 2011 majira ya mchana ambapo lilitokea tetemeko la ardhi la kiwango cha 9.0 katika Pwani ya Sendai, nchini Japan.
Tetemeko hilo likiwa linaendelea, watu kutoka maeneo mbalimbali walirekodi tetemeko hilo na katika office nyingine zenye mifumo ya CCTV tetemeko hilo na athari zake zilirekodiwa.
Majengo marefu sana ya hadi mita 300, ambayo yalikuwa mbali na eneo la ufukwe huo, huko Tokyo pia yalitingishwa. Tetemeko linaelezwa kuchukua dakika tano jambo ambalo wataalamu wa jografia wanasema sio la kawaida.
Kufuatia tetemeko hilo, ardhi ilianza kupasuka kidogo kidogo na maji kuanza kuonekana yakitokea ardhini, hofu ikazidi kutanda. Haya yalianza kutoka kuanzia mida ya saa 7 mchana na baada ya takriban masaa mawili, tsunami kubwa iliikumba nchi hii.
Kutoka kwenye ufukwe huo, tsunami hiyo ilisafiri hadi zaidi ya kilometa 100 nchi kavu. Tsunami hii inatajwa kuwa moja ya tsunami kubwa sana kuwahi kutokea duniani na ni tsunami kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini Japan.
Ripoti ya Shirika la Polisi la Kijapani lilithibitisha vifo vya watu 15,895, huku 6,156 wakijeruhiwa, na watu 2,539 wakiripotiwa kupotea.
Ripoti nyingine ya mwaka 2015 ilionyesha kuwa watu 228,863 waliishi mbali na nyumba yao ama makazi ya muda kutokana na kuharibiwa kwa makazi yao, kulikosababishwa na tsunami hiyo.
Ripoti nyingine ya shirika hilo la Polisi Machi 2018 ilionyesha kuwa majengo 121,776 yalianguka kabisa, huku majengo zaidi ya 280,923 “kuanguka na kuharibika nusu”, wakati majengo mengine 726,574 yaliharibiwa kabisa na tsunami.
Inakadiriwa kuwa tsunami hiyo ilisababisha hasara kati ya Dola za Marekani 14.5 bilioni hadi Dola bilioni 34.6 ambayo ni sawa na Tsh za Kitanzania trilion 34.8 hadi Trilioni 83.04 ambazo ni za kuharifika kwa mali na miundombinu.
“Hata ukikaa Koromije watakuondoa, hili sikubaliani nalo” –Kitwanga