Leo February 6, 2019 nikusogezee kilichojiri katika Mahakama za Tanzania ikiwa ni pamoja na hukumu ya kesi ya waliomuibia kwa kutumia silaha Msanii wa filamu na Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha ambapo Mahakama ya Wilaya Kinondoni imewahukumu miaka 30 jela.
Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa watatu ambao ni Benard Joseph na Yaram Leonard lakini Mahakama iliamua kumfutia kesi mshtakiwa wa tatu Asma Mwaipopo, ambaye aliugua matatizo ya uzazi na kufariki dunia wakati kesi ilipokuwa ikiendelea.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Joyce Mushi, ambapo amesema Mahakama hiyo imejiridhisha na ushahidi uliowasilishwa na mashahidi nane kutoka upande wa mashtaka na kwa sababu ulikuwa na vielelezo vya kutosha.
“Kwa mazingira hayo mahakama hii inawatia hatiani kwa kosa la hilo kutokana na ushahidi wa kina uliowasilishwa hapa na mashahidi hao kutoka upande wa mlalamikaji kwani nimeuthibitisha pasi na shaka,” amesema Hakimu Mushi.
Kutokana na hatua hiyo, amesema kila mshtakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela, ambapo hilo litakuwa ni onyo na fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za wizi wa kutumia silaha.
Washtakiwa hao kwa mara ya kwanza walipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo December 15, 2016 na kwa mujibu wa hati ya mashtaka walitenda kosa hilo November 7, 2016 maeneo ya Mbezi Makonde Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni.
Katika wizi huo inadaiwa waliiba Simu moja aina ya Samsung, Hati ya kusafiria yenye namba 791848, Wallet, USD Dola 1000, Begi dogo, Chaja ya simu na vinginevyo aidha kabla na baada ya kuchukua mali hizo walimtisha Msanii huyo ili kujipatia mali hizo.
Mtanzania kizimbani, kisa Waingereza
Mahakama ya Afrika Mashariki ina Uhaba wa Fedha na Wafanyakazi