Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba amepokea tani 230 za Cement kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari polisi Pemba na Tani 130 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali na mabweni ya wanafunzi katika jimbo la Iramba kutoka kiwanda cha Simba Cement cha jijini Tanga.
Waziri Mwigulu amewashukuru kiwanda hicho kwa kuchangia shughuli za maendeleo ya jamii hasa kusaidia serikali katika ujenzi wa nyumba bora za Askari Polisi na ujenzi wa hospitali pamoja na mabweni na kusema kuwa ni mfano wa kuigwa nchini.
Ameyasema hayo leo February 21, 2018 Tanga katika kiwanda hicho cha Simba Cement na kuwataka Watanzania na wafanyabiashara wenye uwezo kuchangia shughuli za maendeleo nchini kama kujenga vituo vya polisi, nyumba za askari polisi, magereza na zimamoto ili kuwapa morali ya kazi zaidi vijana wanaofanyakazi kulinda raia na mali zao.
Nae Mkurugenzi wa kiwanda cha Simba Cement Mhandisi Reinhardt Swart amesema kama Kampuni huwa wanasaidia sana shule zilizo katika mkoa wa Tanga lakini sasa wameamua kusaidia Taasisi zingine za serikali ambazo zinauhitaji wa kuboresha miundombinu kama wanavyofanya kwa polisi Pemba na shule na hospitali za Iramba.
DC Madusa aagiza Polisi kukamata Wanaojiuza, kuvaa Vimini na Milegezo ili wakafyatue Tofali
Baba Mzazi wa Akwilina aomba kuonana na JPM, amesema ana siku 4 hajaoga