Kwenye list ya nchi ambazo zina uchumi mzuri zaidi Africa, Nigeria imo… YES, yani hata ukizitaja tatu bora nayo imo… Nigeria imetajwa kama nchi yenye uchumi mzuri mwaka 2015 na yenyewe inashika nafasi ya tatu, wakati ya kwanza ni South Africa na ya pili ni Egypt !!
Lakini kama unakumbuka vizuri, September 11 kila mwaka nchi ya Marekani ina kumbukumbu ya tukio la shambulio la Kigaidi lililotokea New York, kwenye Jengo kubwa la Biashara la Kimataifa, World Trade Center mwaka 2001.
Sasa jina la World Trade Center linakuja Africa, Mjengo unashushwa rasmi kabisa katikati ya Jiji la Abuja Nigeria… kitu kitakuwa ni cha kisasa na ndani yake kutakuwa na vyumba vya Biashara pamoja na apartments ambazo watapangishwa watu na watakuwa wanaishi kama home tu yani !!
Unaambiwa mpaka hiki kitu kikikamilika kitakuwa kimeweka Rekodi ya kuwa Jengo kubwa zaidi Afrika Magharibi ambalo ndani yake kuna shughuli za aina nyingi zinafanyika.
Ufunguzi wa Jengo hilo utafanyika mwaka 2016 ambapo awamu ya kwanza ya Ujenzi itakuwa imekamilika.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos