Kampeni ya Ukarimu wa Vodacom kutoka Vodacom Tanzania Foundation ni moja kati ya Kampeni yenye lengo la kuwaweka Watanzania pamoja katika Msimu huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo umefanikiwa kwa 100%.
Ni ukweli kwamba Vodacom Tanzania imefanikiwa kuwafikia zaidi ya Watanzania 20,000 katika msimu huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaoelekea ukingoni ambapo jumla ya tani 4 za tende zimegawiwa kwa Watanzania na maji chupa 25,000 kwa wakazi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na Zanzibar.