Watangazaji sita wanaume wa Shirika la Utangazaji Uingereza BBC wamekubali kukatwa mishahara yao ili kuunga mkono hoja ya kuvunja pengo la kijinsia kwenye kulipwa mishahara baina ya wanaume na wanawake kwenye maeneo ya kazi.
Imezungumzwa na wanaharakati wa kimataifa kuwa Dunia nzima inakabiliwa na tatizo la wanaume kulipwa mishahara mikubwa zaidi ya wanawake kwenye maeneo ya kazi hata kama majukumu yao yanafanana.
Watangazaji hao ni pamoja na Jeremy Vine, John Humphrys, Huw Edwards, Nick Robinson, Nicky Campbell na Jon Sopel. Hii ni kutokana na Mhariri wa BBC nchini China Carrie Gracie kuandika barua ya kuacha kazi wiki chache zilizopita kwa alichodai ni Wahariri wa kiume wa shirika hilo kulipwa zaidi ya wanawake.
Bado viwango halisi vya pesa zitakazokatwa kwenye mishahara ya watangazaji hao havijawekwa wazi lakini wamekuwa wakilipwa kati ya Euro 200,000 hadi 75o,000 ambazo ni kati ya Tsh Milioni 540 hadi Tsh Bilioni 2.02.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana nje ya Mahakama Tido na Kubenea
Polisi Dodoma kuhusu Nabii Tito alivyotaka kujiua