November 30, 2018 Mahakama Kuu ya Tanzania, inatarajia kutoa uamuzi kama itatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ama kukubali kuhusu kufutiwa dhamana kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Hayo yanatarajia kutokea baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha pingamizi wakitaka pingamizi la Warufani hao litupwe.
Uamuzi huo Rufaa hiyo unatarajiwa kutolewa na Jaji Sam Rumanyika baada ya kusikiliza pingamizi la upande wa Jamhuri.
Katika pingamizi lao upande wa Jamhuri umedai vifungu vya kisheria vilivyotumika si sahihi.
Wakili wa Serikali Mkuu, Dk. Zainabu Mango akiwasilisha hoja za pingamizi amedai vifungu vya sheria walivyotumia kuwasilisha rufaa si sahihi hivyo anaomba rufaa itupwe na kuongeza kuwa walitakiwa kuwasilisha rufaa chini ya kifungu cha sheria namba 359 na 361 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai.
Pia wanadai mwenendo wa kesi ulifikishwa Mahakamani haujakamilika na haujachapwa hivyo hausomeki vizuri kwani kuna maneno yamekatika na mwandiko wa Hakimu hausomeki vizuri katika baadhi ya maeneo.
Upande wa Jamhuri unaendelea kuwasilisha hoja huku upande wa warufani ukiongozwa na Wakili Peter Kibatala wakisubiri kujibu.
Katika majibu yake, Wakili Kibatala amedai kuwa hoja za upande wa Jamhuri hazina mashiko kwa sababu Mahakama ilishamalizana na suala la nyaraka.
Kutokana na mvutano wa hoja za kisheria, Jaji Rumanyika, ameahirisha shauri hilo hadi kesho November 30,2018 ili kutoa uamuzi kuhusu pingamizi za Jamuhuri na kwamba kama atatengua uamuzi wa Mahakama ya Kisutu ama lah.
Mbowe na Matiko walifutiwa masharti ya dhamana katika Mahakama ya Kisutu, wiki iliyopita katika kesi inayowakabili pamoja na wenzao ya mashtaka 13 ikiwemo uchochezi.
POLISI WALIVYOWADHIBITI WANACHAMA WA CHADEMA MAHAKAMA KUU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA