Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema ametuma ombi Rais Magufuli kuzungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Luoga kwa kile anachodai kuwa ametoa kauli tata.
Lema ameandika katika ukurasa wake wa Twitter hivi “Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu, kwa maoni yangu Gavana anaongea sana. Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini”
LIVE:Tamko la Mamlaka ya usafiri wa anga juu ya Shirika la FASTJET kufungiwa