Ikiwa zimepita siku 16 tangu kuuawa kwa askari 14 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) waliokuwa kwenye oparesheni ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Husssein Mwinyi amewatembelea wanajeshi wa Tanzania waliopo nchini humo.
Mwinyi alifika nchini humo December 22, 2017 ambapo alipowatembelea Wanajeshi wa Tanzania wanaoshiriki katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani mashariki ya Congo, na kuwatembelea wanajeshi waliojeruhiwa wakati wa shambulizi la December 7, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Beni, Mwinyi ametoa wito wa kudumisha ushirikiano kati ya pande zote zinazoshiriki katika kuleta amani Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Wanajeshi 14 wa Tanzania wa kikosi maalum cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC waliuawa na wengine 44 kujeruhiwa wakati wa majibizano ya risasi na waasi wasiojulikana katika kambi yao huko Semulik, karibu na mji wa Beni.
LIVE: Kutoa heshima za mwisho kwa mashujaa wa JWTZ waliopoteza maisha DRC