Kama unafuatilia kikao cha Bunge toka ulipoanza mkutano wa 18, kumekuwa na swali ambalo limeulizwa zaidi kuhusiana na hatua ambazo Serikali imezichukua kunusuru hali mbaya ya huduma iliyopo katika Hospitali ikiwa ni pamoja na uhaba wa dawa uliosababishwa na bohari ya Madawa MSD kusitisha kutoa huduma hiyo katika Hospitali za Serikali.
Katika kikao cha Bunge leo Dodoma haya ndiyo aliyoyasema Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid >>> “Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nimefanya yafuatayo, nilishaagiza bohari ya dawa kupeleka dawa muhimu zenye thamani ya shilingi milioni mia mbili, nimesitisha ongezeko za tozo zilizofanywa hivi karibuni na Hospitali hiyo’
‘Nimeagiza uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kushughulikia na kurekebisha mara moja mazingira na miundombinu ya Hospitali hiyo ambayo yapo ndani ya uwezo wao… serikali imeendelea na utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya ini kwa wafanyakazi wa afya…“
Hii ni sauti ya Waziri wa afya akizungumza masuala hayo Bungeni Dodoma leo.