Mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) ilitangaza Jumatano mpango wa kuanzisha sheria mpya ambapo mtumiaji mpya nchini New Zealand na Ufilipino, ambao hawalipii uthibitishaji [tiki ya blue]watalazimika kulipa $1 sawa na zaidi ya tsh 2000 kila mwaka ili kutengeneza machapisho au kuwasiliana na wengine.
Watumiaji waliopo ambao tayari wana akaunti za X hawataathiriwa na programu ya‘Not a Bot’, ilisema Timu ya Usaidizi ya X.
Watumiaji wapya ambao hawalipi wataweza tu kutazama machapisho ya watu wengine.
Chapisho la X halielezi kwa nini usajili mpya wa $1 ni wa watumiaji wapya wanaojiunga kupitia wavuti pekee na wala si programu ya simu, au kwa nini Not a Bot inatolewa katika nchi mbili pekee.
Mpango huu mpya ni pamoja na usajili mkuu wa mtandao wa X wa $8 sawa na Tsh 20,000 kwa mwezi.