Ushahidi wa kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwanahisa wa mtandao huo, Micke William umekwama kuendelea kutokana na shahidi kutoandaliwa.
Pia sababu nyingine ya kukwama, ni upande wa mashtaka kueleza jalada lipo Polisi huku Mawakili wa Serikali wanaosikiliza kesi hiyo kuwa na kesi nyingine kwa Mahakimu tofauti.
Wakili wa Serikali Nasoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi October 17, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Video ya Manji akirudi Mahakamani Saa 96 baada ya kuachiwa huru
Ulipitwa na hii? BREAKING: Mahakama ya Kisutu imemuachia huru Yusuf Manji