Idara ya Uhamiaji imeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya kuishi nchini bila Visa inayomkabili Raia wa Uholanzi, Monique Amanzi mwenye umri wa miaka 28, umekamilika.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Uhamiaji, Novatus Mlay mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.
Mlay amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali mshtakiwa, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi October 25, 2017.
Mshtakiwa anadaiwa kuwa September 11, 2017 akiwa Uhamiaji Makao Makuu, Kurasini Temeke alikutwa bila kuwa na visa kinyume na sheria.
KILIMANJARO: Polisi wamuua jambazi sugu, kakutwa na simu 19 na line 58