Daktari Bingwa wa Tiba za Moyo wa Hospital ya Aga Khan, Prof. Mustapha Bapumia (63) leo September 25, 2017 ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangazwa kuona Mfanyabiashara Yusuf Manji kuwa na vyuma vinne katika moyo wakati ni kijana mdogo.
Aidha, Prof Bapumia ameieleza Mahakama hiyo kwamba Manji anayekabiliwa na kesi ya dawa za kulevya, anapaswa kujiangalia kwa sababu anaweza kukumbwa na umauti muda wowote licha ya kuwa hiyo ni mipango ya Mungu.
Prof. Bapumia ambaye ni Shahidi wa tatu katika kesi hiyo, ameyaeleza hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha na kudai kuwa anashangaa mtu mwenye umri mdogo kama huo kuwa na vyuma vinne kwenye moyo kitaaluma lazima ajiangalie sana.
Katika ushahidi huo akiongozwa na Wakili wa utetezi Hajra Mungula, alidai kuwa ana PHD ya Adiology ambaye ni Prof. Msaidizi wa Adiology wa Aga Khan.
Alidai kuwa February 21, 2017, Manji alifikishwa Hospital hapo akiwa anasumbuliwa na maumivu kwenye moyo ambapo alipelekwa kwenye kitengo cha dharura ambapo amesema ana tatizo sugu la moyo na umri wake ni mdogo na kwamba aliwahi kuzibuliwa mishipa mitatu ya moyo katika nchi za India, Dubai na Marekani lakini pia bado alikuwa akipata maumivu.
Aliendelea kudai baada ya kufanyiwa uchunguzi ilionekana kuna mshipa mwingine ulioziba licha ya iliyozibuliwa kuwa wazi lakini aliomba apewe dawa kwa sababu familia yake na matibabu yake yapo Marekani.
Baada ya kumfanyia vipimo walimshauri kutumia dawa za aina nne ambazo ni muhimu sana kwa sababu ya umri wake mdogo kwa ajili ya kupunguza maumivu makali.
Aidha, amedai kuwa Manji ana maumivu sugu ya mgongo na kukosa usingizi ambapo alipewa dawa za kupunguza maumivu (Benzodiazepines) ambazo zinatolewa kwa cheti cha daktari.
Alisema Manji hakupata muda wa kukaa nyumbani ambapo tatizo lilijirudia na kurudishwa tena February 24, 2017 saa mbili usiku hospitalini hapo na walivyompokea vipimo vilionyesha amepata mshtuko tena wakarekebisha na kumuwekea chuma na kuruhusiwa March 14, 2017.
>>>”Sisi kwa wagonjwa wa moyo tunatumia Morphine ambayo inasaidia kupunguza maumivu makali na dawa kutoka nje zinaruhusiwa lakini ukiwa na mzigo mkubwa lazima uwe na kibali cha TFDA.”
Naye Shahidi wa nne katika kesi hiyo, Dr Khan aliieleza Mahakama kuwa yeye ni daktari wa watoto na familia na amekuwa akimtibu Manji toka aliwa na miaka mitatu.
>>>”Kwanzia 1978 akiwa na miaka mitatu nilikuwa namtibu yeye na familia yake kwa ujumla ambapo alikuwa akimtibu matatizo mbalimbali.”
Alidai Manji alikuwa akienda hospitalin kwake mara zaidi ya mara tatu na hajawahi kuona kiashiria cha kutumia dawa za kulevya.
Dakika 215 za Yusuph Manji kujitetea kesi ya dawa za kulevya leo
Yusuf Manji baada ya Mahakama ya Kisutu kumuachia huru