Naibu Spika Dr. Tulia Ackson akiwa Mgeni Rasmi wakati wa uchangishaji fedha za vikundi vya wanawake Mkoa wa Songwe aliwashutumu baadhi ya Wabunge wasiotekeleza ahadi zao lakini hukasirika wanapoona mtu mwingine akifanya waliyoshindwa kuyafanya.
Katika zoezi hilo ambalo lililoandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Juliana Shonza jumla ya Tsh. Milioni 32 zilipatikana ambapo katika hotuba yake Dr. Tulia alisema:>>>”Tupo Wabunge kadhaa ambao hatufanyi yale ambayo tuliwaahidi Wananchi wetu na wakati mwingine anapofanya mtu mwingine yale tuliyowaahidi Wananchi tunakasirika.
“Nawaomba Wabunge hasa wa Chama Cha Mapinduzi kuiga mfano mzuri wa Mheshimiwa Shonza wa kutekeleza kwa kutekeleza ahadi wanazozitoa kwa Wananchi wakati wa kupigiwa kura.” – Dr. Tulia.
Zaidi unaweza kumtazama kwa kuplay hii video hapa chini…
Kitu Zitto Kabwe ameongea mbele ya Rais Magufuli Kigoma…play kwenye hii viedo hapa chini kutazama!!!