Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Thomas Justice Daffa Machupa amewataka wazazi na wananchi kujitoa kwaajili ya kuboresha miundombinu ya Shule za Sekondari na msingi ili kukuza Elimu ya watoto wao.
Katibu Daffa ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Celina Kombani iliyopo kata ya mwaya wilayani humo.
Aidha Daffa ameipongeza shule hiyo kwakuondoa ziro na kupandisha ufaulu mwaka hadi mwaka jambo ambalo ni sifa njema kwa wilaya kwa ujumla na kuwaahidi kuzishughulikia changamoto zinazowakabili ili kuongeza ufanisi zaidi katika ufundishaji.
Kwa upande wake makamo mkuu wa shule hiyo ya celina kombani amesema wanachangamoto kubwa ya vifaa vya ufundishaji,Nyumba za walimu,kukosekana kwa uzio na gari ya dharura pale inapotokea jambo kwa wanafunzi hususani wale wanaoishi kwenye mabweni.
Shule ya celina kombani ilifunguliwa rasmi tarehe 20/06/2007 na hayo ni Mahafali ya 13 ya kidato cha nne tangu shule hiyo kuanzishwa.