Leo September 26, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeukubalia upande wa mashtaka kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka katika kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo (40) na mwenzake.
Mbali ya Melo mshtakiwa mwingine ni Mwanahisa wa mtandao huo, Mike Mushi.
Ombi hilo limekubaliwa, baada ya Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi kumueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwamba wanaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka licha ya kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
Kishenyi amedai wanaomba kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka, chini ya kifungu 234 (1) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai( CPA).
Kutokana na hatua hiyo, Wakili wa utetezi, Jeremiah Ntobesya, alipinga maombi hayo kwa madai kuwa tayari Mahakama imeshasikiliza shahidi mmoja wa upande wa mashtaka.
Hata hivyo, Hakimu Simba alisema anakubaliana na ombi hilo, hivyo ameahirisha kesi hiyo hadi October 11, kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
PROF. TIBAIJUKA: ‘Mimba za ubakaji zipo lakini mbakaji anaangalia saikolojia ya mtoto’