Jumapili September 17, 2017 Chelsea imeshindwa kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani Stanford Bridge baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Arsenal katika mchezo wa muendelezo wa Ligi Kuu ya England maarufu kama EPL.
Katika mchezo huo, Chelsea walijikuta wakicheza pungufu katika dakika tatu za mwisho baada ya mlinzi wake wa kati David Luiz kuoneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Michael Oliver kwa kumchezea vibaya Sead Kolasinac.
Kwa matokeo haya Arsenal imeizuia Chelsea kushinda mfululizo kwenye mechi za Premier League wanapokutana Stamford Bridge. Chelsea wanasalia katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 10 baada ya michezo mitano wakati Arsenal wanakamata nafasi ya 12 wakiwa na pointi 7 baada ya mechi tano.
Video ya dakika 3 ya magoli ya Taifa Stars vs Botswana September 1 2017, Full Time 2-0