Wiki iliyopita, Daktari wa timu ya mazoezi ya viungo Marekani Larry Nassar alihukumiwa kifungo cha miaka 175 jela baada ya kukutwa hatia ya makosa ya ukatili wa kingono dhidi wanawake wanamichezo.
Katika kesi hiyo walijitokeza mashahidi 160 kuwasilisha ushahidi wao dhidi yake na hadi wakati huo alikuwa tayari akitumikia kifungo cha miaka 60 kwa kukutwa na hatia ya kumiliki picha za ngono za watoto kinyume cha sheria.
Hatahivyo Jaji katika jimbo la Michigan jana ameeleza kuwa idadi ya waathirika hao wa unyanyasaji wa kijinsia yaliyofanywa na daktari huyo imeongezeka mpaka kufikia 265.
Dr. Nassar hivi karibuni atafikishwa tena mahakamani kwa makosa ya kudhalilisha wagonjwa katika chumba cha nyuma cha klabu ya mazoezi ya viungo huko Michigan.
‘Ni kosa kufungisha Ndoa kama Haujasajiliwa’ – Jane Barongo