Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania kwa kushirikiana na TAKUKURU wamebaini vyeti feki zaidi ya 100 katika Idara hiyo.
Raisi wa Chama hicho Godfrey Hongoli amesema kwa kushirikiana na TAKUKURU wameweza kubaini vyeti feki zaidi ya 100 katika idara hiyo ambapo tayari mtu mmoja ameshafungwa miaka saba.
Aidha, amesema mbali na hayo, wanakabiliana na wimbi wa Maabara za Afya ambazo hazijasajiliwa hivyo kuhatarisha ustawi wa sekta hiyo nchini.
Rekodi nyingine ya Mtanzania aliyepata udhamini kusoma Harvard University