Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Wizara ya Afya, inakusudia kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mpaka kufikia 2020 ili kutokomeza vifo vya wajawazito na watoto wachanga nchini.
Akizungumza baada ya kukutana na Wakuu wa Idara na vitengo mbalimbali kwa ajili ya utambulisho wa Naibu Waziri Dr. Faustine Ndungulile katika Ofisi ndogo za Wizara hiyo, Dar es salaam, Waziri Ummy amesema>>>”Vifo vya wajawazito vimekua tishio nchini, hivyo ni lazima tuimarishe huduma za afya ya mama na mtoto ili tufikie malengo ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi mpaka kufikia 2020 ili kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora.”
Aidha, Waziri Ummy amesema katika kuboresha hilo amewaagiza Wakuu hao wa Idara katika Wizara ya Afya kushirikiana na mfuko wa bima ya afya nchini (NHIF) kuona iwapo upo uwezekano wa kuanzisha bima ya afya kwa wajawazito kwa bei nafuu hadi kufikia July Mosi, 2018.
Waziri Mpina kaanza na MNADA wa ng’ombe zaidi ya 1,000 kutoka Kenya
MWANZA: Akamatwa akijifanya mtumishi wa Jiji na kukusanya ushuru