Baada ya kusota Mahabusu kwa siku nne, Vigogo wawili wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wanaokabiliwa na kosa la kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 1,097,681,107, wameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Vigogo hao ni aliyekuwa Kaimu Mtendaji Mkuu, Shaha Hanzuruni na Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Onesphor Luhungu.
Masharti waliyotimiza ni kuwa na wadhamini wawili kila mmoja na kusaini bondi ya Tsh. Milioni 250 ambazo zimetakiwa kupelekwa Mahakamani hapo.
Washtakiwa hao pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiria Mahakamani na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila kibali cha Mahakama ambapo baada ya kutimiza masharti hayo, kesi hiyo iliahirishwa hadi October 24, 2017.
Wawili hao wanakabiliwa na kosa la matumizi mabaya ya madaraka January 1, 2012 na December 30, 2014 katika Ofisi za TIA zilizopo Temeke wakiwa wafanyakazi wa Chuo hicho, mmoja akiwa Kaimu Mtendaji Mkuu na mwingine Mkuu wa kitengo cha fedha hawakufuata taratibu za manunuzi ya kununua ardhi kampasi ya Mwanza na kusababisha Vedastus Lukago kupata faida ya Bilion 1,097,681,107.
Katika kosa jingine inadaiwa wameisababishia Mamlaka hasara kati ya January 1, 2012 na December 30, 2014 kwa nafasi zao na matendo yao walisababisha hasara ya Bilioni 1,097,681,107 fedha za TIA.
MWANZA: Hiace kuzama Ziwa Victoria na kuua 12…tazama kwenye hii video hapa chini