Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho, Said Mrisho inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion imeahirisha hadi October 12, 2017.
Kesi hiyo imeahirishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na Hakimu Mkazi Flora Haule kupata dharula.
Wakili wa Serikali, Ester Kyala ameeleza kuwa anaomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu Wakili anayesikiliza kesi hiyo yupo Mahakama Kuu pamoja na Wakili wa mshtakiwa, Juma Nassoro ambapo baada ya kuelezwa hayo, kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017.
BREAKING: Hiace yazama Ziwa Victoria na kuua 12, Shuhuda na RPC wasimulia