MLINZI wa Klabu ya Barcelona Gerard Pique amesema atastaafu soka la Kimataifa kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2018 endapo itathibitika kuunga kwake mkono Uhuru wa Jimbo la Catalonia ni tatizo.
Barcelona iliichapa Las Palmas mabao 3-0 katika uwanja ambao haukuruhusiwa kuingiza mashabiki Jumapili kufuatia maandamano yaliyokuwa yakiendelea katika Jiji hilo ambapo Pique akisema huo ulikuwa mchezo mgumu zaidi kwake.
>>>”Nadhani, naweza kuendelea, lakini kama Bodi itadhani mimi ni tatizo, itaachana na timu ya Taifa kabla ya 2018. Wapo watu wengi Uhispania ambao hawakubaliani na kilichotokea na kuamini katika demokrasia.”
Catalonia, sehemu yenye watu wapatao Milioni 7.5 kaskazini-mashariki mwa Uhispania, ina lugha yake na utamaduni wake huku Barcelona ukiwa Mji wake Mkuu lakini haitambuliki kama nchi huru bali ni sehemu tu Uhispania kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.
Pique ameichezea Uhispania mechi 91 lakini ameonekana mtu wa tofauti bada ya kuunga mkono kura ya maoni ya kujitenga kwa Catalonia ambapo kabla ya mchezo dhidi ya Las Palmas Jumapili, aliposti picha kwenye Twitter akiwa anapiga kura na kuandika: “Nimeshapiga kura tayari. Kwa pamoja hatuzuiliki kulinda demokrasia.”
Sababu za game ya Barcelona vs Las Palmas kuchezwa bila mashabiki