Jumanne October 3, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mhasibu wa Shule ya Sekondari St. Joseph Cathedral, kwenda jela miezi 12 au kulipa faini ya Tsh Milioni 5 baada ya kutiwa hatiani katika kosa la kumuita Rais Magufuli kilaza kupitia mtandao wa WhatsApp.
Hata hivyo, Mhasibu huyo ameepuka kwenda gerezani kutumikia adhabu baada ya kulipa faini hiyo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema amesikiliza ushahidi wa pande zote mbili ambapo upande wa Jamhuri uliita mashahidi saba kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.
>>>”Mahakama hii inakutia hatiani dhidi ya mashtaka yanayokukabili, ambapo utalipa faini ya Tsh. Milion 5 na ukishindwa kulipa faini utatumikia kifungo cha miezi 12, jela.”
Awali, kabla ya hukumu hiyo, mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ili apunguziwe adhabu ambapo alidai mama yake mzazi ni mzee anamtegemea na ana watoto na familia nzima inamtegemea.
Katika kesi ya msingi, mhasibu huyo anadaiwa August 6, 2016 akiwa anajua aliwasilisha maneno kinyume cha sheria kupitia mtandao wa WhatsApp katika group la wafanyakazi la STJ kwa nia ya kumtusi Rais.
Mshtakiwa alinukuliwa “Habari za asubuhi humu hakuna Rais kilaza kama huyu wetu duniani angalia anavyompa Lissu umashuhuri, fala yule picha yake ukiweka ofisini nuksi tupu ukiamka asubuhi ukikutana na picha yake kwanza siku inakua ya mkosi mwanzo mwisho.”
“Sikuja kuuza sura nilipendwa na mke wangu inatosha” – Rais Magufuli