Jumatatu September 25, 2017, Mfanyabiashara Yusuf Manji ametumia dakika 215 ambazo ni zaidi ya saa tatu kujitetea katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwa ni siku ya kwanza kati tatu zilizopangwa kusikiliza ushahidi wake.
Mbali ya Manji, pia Daktari wa Hospital ya Agha Khan, Profesa Mustapha Bapumia ameeleza kuwa Manji ana vyuma vinne kwenye moyo wake na hivyo anatembea kwenye kamba nyembamba akisema mfanyabiashara huyo ana tatizo sugu la moyo licha ya umri wake kuwa mdogo.
Aidha, amesema kwamba walipoangalia kwenye historia ya matibabu yake, wamegundua amezibuliwa mishipa ya moyo wake Dubai, India na Marekani.
Katika utetezi wake Manji akiongozwa na Wakili wake, Hajra Mungula amemueleza Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha kwamba anafanya kazi ya ushauri wa Kampuni za kifamilia.
Manji: Sijatendewa haki na sijasikikizwa mbele ya mahakama.
Manji: Dawa ambazo zinatajwa kwenye hati ya mashtaka, Morphiem na Benzodiazepines ni sehemu ya dawa zangu ninazotumia.
Manji: Nilitumia dawa hizo hata siku niliyohojiwa Polisi, hivyo nimechafuliwa sana katika jamii kwani hizo dawa nina uthibitisho wake.
Manji: Napenda kutoa uthibitisho wa nyaraka za maelezo ya Daktari wangu kutoka Marekani kuhusu dawa hizo.
Manji: Uthibitisho wa nyaraka hizo ulifika kwa njia ya e-mail na sekretari alitoa nakala wakati nikiwa Hospital ya muhimbili.
Manji: Historia yangu ya kiafya aya matatizo ya moyo yapo katika ukoo wetu, ambapo nilianza kusumbuliwa nikiwa na miaka 26.
Manji: Wakati nakojoa kwa ajili ya kuchukuliwa sampo ya mkojo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, mlango ulikuwa wazi na nilikabidhi sampo kwa mtu aliyekuwa nyuma yangu.
Manji: Wakati sampo ya mkojo inachunguzwa sikuulizwa, wala uchunguzi haukufanyika mbele yangu.
Manji: Baada ya kutolewa sampo ya mkojo walienda kukagua nyumbani kwangu ambapo walichukua Kompyuta, Viza Card, Simu, Credit Card, Bima na saa ambapo hadi leo Polisi hawajamrudishia.
Manji: Nashangaa nakabiliwa na kesi ya dawa za kulevya lakini Polisi wamechukua vitu vingine ambavyo havihusiki na hadi leo hawajanirudishia.
Manji: Hii kesi ni propaganda na inatokana na ugomvi wa kibiashara na ni mchezo mchafu, kwani hakuna asiyejua kama alikuwa anagombania Kampuni ya Tigo.
Manji: Hii kesi imenisababishia athari kubwa sana, binafsi Baba yangu alinieleza vitu 2 ambavyo ni jina zuri na maadili katika jamii.
Manji: Nimejiuzulu klabu ya Yanga kwa sababu ya dawa za kulevya na niliandika barua kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke kuachia udiwani.
Manji: Nakumbuka February 8, 2017 nilipata taarifa saa 7 mchana kupitia e-mail yangu kwamba mimi ni muuzaji wa dawa za kulevya na Ijumaa February 10 nahitajika kwenda kwa ZCO.
Manji: Kutokana na taarifa hiyo aliitisha mkutano na waandishi wa h hábari na kukanusha taarifa hiyo, ambapo February 9, 2017 aliamua kuripoti mwenyewe Polisi.
Manji: Niliamua kuwahi polisi mwenyewe kwa sababu naiheshimu jamhuri, hivyo nikaona niwafate mimi kwani nilitaka hayo mambo yaishe mapema.
Manji: Hivyo niliamua kujiuzuru Yanga kwa sababu watu wangewacheka wachezaji na wanachama wa Yanga, kwamba Mwenyekiti wao anatumia dawa za kulevya.
Manji: Nilipelekwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, saa 11 jioni ambapo nilikutana na Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima.
Manji: Baada ya kufika kwa Mkemia niliomba ruksa ya kuvuta sigara ambapo baada ya nusu saa tulielekezwa sehemu na kupewa chupa na kukojoa.
Manji: Hivyo hizi tuhuma zimeniaribia sana, kwani nilishindwa kwenda hata msikitini. Imeniaribia sifa, biashara hata ninaoshirikiana nao nje ya nchi wananiuliza.
Manji: Biashara aliianzisha baba yangu tangu mwaka 1975 ambapo baadaye nilirithi uongozi na mwaka 2016.
Manji: Heshima yangu imeshuka hata mbele ya viongozi wakubwa akiwemo Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Raila Odinga ambao wananifahamu, hivyo naona aibu.
Manji: Wakati wa kujazwa kwa fomu ya mkojo kwa mkemia mkuu wa Serikali sikushirikishwa.
Manji: Baada ya kutoka hospital ya Agha Khan nilimwambia Mwanasheria wangu aandike barua ya kuomba majibu ya mkemia kuhusu vipimo vya mkojo.
Manji akiendelea kuongozwa na Wakili Mangula, aliulizwa kama alishawahi kupata elimu ya madawa alijibu kuwa hajasomea.
Manji: Uelewa juu ya madawa nimeupata kwenyé timu ya mpira, alipougua baba yangu mzazi nilikuwa naenda naye hospital.
Aidha Manji alipoulizwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Timony Vitalis kwamba anajua dawa za kulevya zinakaa muda gani mwilini alijibu ndio.
Vitalis: Manji uliomba vibali vya kutumia dawa zako ambazo nchini hazipo?
Manji: Ingekuwa biashara ningeomba, lakini hizi natumia kama dawa hivyo zinakibari na uthibitisho maalum kutoka hospitali niliyopewa.
Vitalis: Uliwahi kupewa onyo la kutovuta sigara?
Manji: Ndio ila nimejaribu kuacha bila mafanikio.
ULIPITWA? Video ya Manji akirudi Mahakamani Saa 96 baada ya kuachiwa huru
Yusuf Manji baada ya Mahakama ya Kisutu kumuachia huru