Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya shughuli ya ndoa kukamilika lakini watu zaidi ya 40 walilazimika kwenda hospitali baada ya kuugua ghafla wakidaiwa kula chakula chenye sumu.
Familia ya mzee Abasi inayoishi katika Halmashauri ya Wilaya Misenyi imemaliza vibaya harusi ya vijana wao wawili waliokuwa wanafunga ndoa baada ya wageni waalikwa pamoja na mabwana harusi kulazimika kuwahishwa Hospital wakidaiwa kula chakula chenye sumu.
Ayo TV na millardayo.com zimewaata mama wa vijana hao wawili, Aida Abasi pamoja na ndugu yao Sharifa Adam na wameeleza kila kitu kilichotokea wakisema kulikuwa na chakula kilichotengwa kwa ajili ya wageni waalikwa pamoja na mabwana harusi lakini baada ya kupata chakula hicho hali zao zilianza kuwageuka kitendo kilichopelekea kufikishwa hospitali pamoja na wageni zaidi ya 40.
SHAMBULIZI LA CHUI: Majeruhi asimulia alivyonusurika kuuawa