Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana makazi ya kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na athari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.
Lowassa na viongozi wengine walivyouaga mwili wa Mke wa Kingunge