Baada ya utawala wa miaka 22 wa kocha Arsene Wenger ndani ya club ya Arsenal na nafasi yake kutangazwa kuchukuliwa na kocha Unai Emery, sasa ni zamu ya usajili.
Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery chini ya utawala wake katika club ya Arsenal, leo wametangaza kumsajili beki wa kulia wa Juventus Stephan Lichtsteiner kama mchezaji huru.
Stephan Lichtsteiner mwenye umri wa miaka 34 amesajiliwa na Arsenal lakini bado haijajulikana ni nani anafuata baada ya Stephan Lichtsteiner, Arsenal kwa sasa ina kocha mpya Unai Emery aliyejiunga nao akitokea PSG ya Ufaransa.