Leo November 2,2018 tunayo story kuhusu taarifa zinazodai kuwa Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Reoland van de Geer ametakiwa kuondoka nchini ifikapo November 3, 2018.
Ayo Tv imezungumza na Afisa Habari wa Umoja wa Ulaya, Sussanne Mbise ambapo amesema kuwa hawana taarifa kuhusu madai hayo ya kufukuzwa kwa Balozi huyo isipokuwa wanafahamu ameitwa Makao Makuu kwa ajili ya kushauriana masuala ya kisiasa.
“Nimesikia kuhusu hayo madai lakini ukweli ni kwamba ameitwa kwenye makao makuu kwa ajili ya kushauriana kwa wiki nzima ijayo, watakuwa wakiongelea kuhusu masuala ya kisiasa ya sasa na uhusiano wa baadae wa European Union na Tanzania,”
Hizi ndio sababu za ZITTO KABWE kuachiwa kwa dhamana