Waziri wa uchukuzi na mawasiliano mhandisi Izak Kamwelwe amesema shirika la ndege la Tanzania la (ATCL) limedhamiria kujiimarusha katika sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya ndege lakini pia kuhakikisha linafika katika nchi mbalimbali barani Afrika na bara la Asia kwa ujumla.
Kwa upande wake waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira na kaimu waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia Kafwaya Mutotwe baada ya ndege ya ATCL aini ya AIRBUS A 220-300 wamesema kuanza kwa safari hizo kutasaidia kuimarisha uhusiano uliopo wa muda mrefu baina ya nchi hizo katika Nyanja mbalimbali.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati ndege aina AIRBUS ilipoanza safari zake katika nchi hizo kwa mara ya kwanza ikianzia nchini Zimbabwe na Zambia ambapo uzinduzi rasmi wa ndege hiyo umefanyika katika viwanja viwili tofauti kikiwemo kile cha Robert Gabriel Mugabe Harare- Zimbabwe na baadae uwanja wa Kenneth Kaunda Lusaka- Zambia, abiria hao wamepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza katika sekta ya anga ambayo zaidi ya miaka ishirini ilionekana kuyumba.
Yalivyohitimishwa mafunzo ya porini ya kijeshi kwa Askari 2000 (JWTZ)