Moja kati ya stori ambazo nimekutana nazo mtandaoni ni pamoja na hii kutoka mtandao wa face2faceafrica.com ambao umetaja nyimbo kumi bora za muda wote, face2faceafrica.com umetaja nyimbo kumi bora za muda wote Afrika, hii ndio list yenyewe.
10- 2face Idibia– African Queen, huu ni wimbo ambao ulitoka 2004 na maudhui ya wimbo huo yalilenga kuwafanya wanawake wa Afrika kujivunia na kujiona wanathamani, huu ni wimbo ambao hadi sasa unatajwa kama miongoni ya nyimbo bora za Afrika za muda wote.
9-‘Nomakhanjani’ ya Brenda Fassie (Afrika Kusini) Marehemu Brenda Fassie alitoa wimbo huo mwaka 1999 na ndio wimbo uliokuwa umebeba jina la Album yake na kwa upande wa Tanzania ni wimbo ambao ulikuwa unapigwa sana kwenye maharusi.
8- ‘Malaika’ wa Fadhili Williams (Kenya) wimbo wa Malaika ni wimbo bora kuwahi kurekodiwa au kuimbwa na msanii kutokana Kenya marehemu Fadhili Williams ambapo ulitoka mwaka 1963 lakini huu ni moja kati ya nyimbo zinazopendwa hadi leo na baadhi ya wasanii wamewahi kuufanyia cover wimbo huo.
https://youtu.be/8siIAxxDuDQ
7- ‘Once a Slave’ ya Monkz ft Maulana (Ghana) unawezekana usiwe wimbo maarufu sana kwa Afrika Mashariki lakini kwa upande wa nchi za Afrika Magharibi huu ulikuwa ni wimbo maarufu sana ukizingati na maudhui yake yanalenda Afrika ambayo iliwahi kutawaliwa na wakoloni ila wimbo huu ulitoka 2006.
6- ‘Mezez Alew’ wa Aster Aweke (Ethiopia) huu ni wimbo ambao ulitolewa miaka ya 90 lakini pamoja na kuimbwa katika lugha ambayo haijazoeleka kuzungumzwa katika nchini, melodi ya wimbo huo na umahiri wa uimbaji wa Aster Aweke ulifanya wimbo huo kuwa mkubwa na ulilenga kuhamasisha watu kufanya ngono salama ili kuepuka HIV.
https://youtu.be/9sU_NYRlAp0
5- ‘Zamina Mina (Zangalewa)’ huu ni wimbo ambao uliimbwa Golden Sounds na kusababisha kupata heshima kubwa nchini kwao Cameroon na kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na mashahiri ya wimbo huo, ulitoka 1986, wimbo huo ulirudiwa tena na wasanii mbalimbali akiwemo Shakira na kuimbwa katika fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.
https://youtu.be/fLys8SapVtA
4- ‘Coupe Bibamba’ wa Awilo Longomba (Congo) mwaka 1998 Awilo ndio alitoa wimbo wa “Coupe Bibamba” wimbo ambao ulimfanya kuwa maarufu nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, kitu cha kipekee ambacho hadi leo kilikuwa kinamtofautisha kirahisi Awilo na wasanii wengine ni kuwa alikuwa na style yake ya kupiga kelele.
https://youtu.be/6a6KHE2ICqg
3- ‘Premier Gaou’ wa Magic System (Ivory Coast) kama ni shabiki muziki najua utakuwa unakumbuka moja kati ya nyimbo zilizotoka mwaka 2002 na kufanya vizuri basi wimbo wa “Premier Gaou” ulikuwa ni moja kati ya nyimbo zilizofanya vizuri barani Afrika.
2- ‘Wombo Lombo’ wa Angelique Kidjo (Benin) huu ni wimbo ambao ulitoka mwaka 1996 na uliimbwa na Angelique Kidjo kutokea Benin, wimbo huo ulikuwa mkubwa sana Afrika hususani katika nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa.
1- ‘Umqombothi’ wa Yvonne Chaka Chaka (South Africa) ni moja kati ya wanamuziki wenye heshima kubwa Afrika Kusini na Afrika kwa ujumla hii inatokana na kudumu kwake kwenye muziki kwa muda mrefu huku akifanya vizuri.
https://youtu.be/P0Duo-4qXMM
Linah Kafunguka “Napenda wanaume weusi, nikiwaona nasisimka, wamekaa kiume”