Imethibitika kuwa mshambuliaji wa kimataifa wa England na club ya Tottenham Hotspurs Harry Kane hatochukuliwa hatua zaidi za kinidhamu na chama cha soka England FA kufuatia tukio lake la kukorofishana na Cesar Azpilicueta wa Chelsea wakati wa mchezo dhidi ya timu zao.
Chelsea na Tottenham Hotspurs zilicheza mchezo wao wa Ligi Kuu England uliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge na kushuhudia Chelsea ikipata ushindi wa magoli 2-0, Harry Kane alipishana na Cesar Azpilicueta na alimsukuma kwa kichwa kama anataka kumpiga hivi, tukio ambalo wengi walidhani anaweza akaadhibiwa zaidi.
FA walikuwa wanasubiria ripoti refa Andre Marriner aliyechezesha mchezo huo kama aliona tukio hilo au la lakini ukweli ni kuwa Harry Kane hawezi kupewa adhabu zaidi kufuatia kitendo chake cha kumsukuma kwa kichwa Cesar, hivyo Kane anafanikiwa kuepuka adhabu ya kufungiwa mechi tatu na atakuwa sehemu ya mchezo wa Arsnal dhidi ya Tottenham weekend hii.
https://youtu.be/aj7W3AeinC0
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake