Kiungo wa club ya Man City na timu ya taifa ya Ujerumani Leroy Sane leo ameripotiwa na vyombo mbalimbali barani Ulaya kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kinachotarajia kucheza na Peru siku ya Jumatano ya wiki ijayo.
Leroy Sane mwenye umri wa miaka 22 ameripotiwa kufikia maamuzi hayo kwa sababu zake binafsi ambapo chama cha soka cha Ujerumani hakijataja sababu ya moja kwa moja.
Baada ya maamuzi hayo wengi wamehusisha kuwa Sane inawezekana kajiondoa katika kikosi cha Ujerumani kwa sababu ya kuachwa na kocha Joachim Low katika kikosi cha wachezaji 23 walioshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Hivyo kuripotiwa leo kujitoa timu ya taifa kwa sababu binafsi kumeanza kuhusisha kuwa inatokana labda na kinyongo kwa kocha Joachim Low ambaye amemuita sasa kwa ajili ya game za UEFA Nations League, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ujerumani aliishia hatua ya makundi World Cup 2018.
Mtazamo wa Madee kwa nini Messi na Griezmann hawakustahili tuzo za FIFA