Club ya Cardiff City iliyokuwa imemsajili Emiliano Sala kutokea Nantes FC ya Ufaransa lakini alipata ajali na kupoteza maisha January 21 akiwa hajaanza kuitumia timu hiyo, imepanga kuanza mpango wa kukusanya ushahidi ili imshitaki wakala Willie McKay ambaye anatuhumiwa kuongeza dau la usajili wa Emiliano Sala.
Willie McKay ambaye ni wakala wa wachezaji soka anatuhumiwa na uongozi wa Cardiff City kusababisha dau la usajili wa Emiliano Sala kutoka Cardiff City kwenda Nantes FC kufikia Pound milioni 15, kitu ambacho kidaiwa kwa kiasi kikubwa kusababishwa na wakal huyo.
Cardiff wanakusanya ushahidi wa kina ili kumshitaki Willie McKay au kuepuka kuilipa Nantes FC kiasi cha Pound milioni 15, mmiliki wa club hiyo mwenye asili ya Malaysia Vincent Tan amegundua kuwa kuna vitu vilienda kinyume na taratibu katika dili la mchezaji huyo.
Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera kataja walichozidiwa wachezaji wake na Simba