Club ya Simba SC kesho saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki watacheza mchezo wao wa kwanza wa round ya kwanza ya CAF Champions League dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland, game itachezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo kocha wa makipa wa Simba SC Mwalami Mohamed ameongea na waandishi wa habari kwa niaba ya kocha mkuu Patrick Aussems na kueleza kuwa wamejiandaa vizuri na kikosi chao kipo kamili ila kitawakosa wachezaji wawili kwa majeruhi Asante Kwasi na Shomari Kapombe anayetibiwa Afrika Kusini pamoja na Juuko aliyepata matatizo ya kifamilia.
“Tunawaheshimu wapinzani wetu japo hatuwajui vizuri lakini kwa maandalizi ambayo tumeyafanya nafikiri tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tuna matatizo kidogo tuna majeruhi ya mchezaji wetu Kapombe, Kwasi na tuna Juuko ambaye alienda timu ya taifa lakini amepata matatizo ya kifamilia na kushindwa kurudi kwa wakati”>>> Mwalami Mohamed
Baada ya mchezo huo siku chache zijazo Simba italazimika kusafiri hadi Mbabane Swaziland kucheza game ya marudiano dhidi ya timu hiyo, ambapo matokeo ya kesho ndio yatawapa taswira ya safari yao ya kuwania kuingia hatua ya makundi ya michuano ya CAF Champions League msimu wa 2018/2019.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?