Moja kati ya stori zilizochukua headlines wakati wa mchezo wa Simba dhidi ya Yanga jana uwanja wa Taifa Dar es Salaam ni ishu ya imani za kishirikina ambazo zilidaiwa kuhusika ili Yanga asifungwe na Simba kutokana na kuelemewa.
Baada ya hapo wengi wakahusisha kitendo cha Ibrahim Ajib wa Yanga kuanza mpira kwa kuutoa nje ni kutokana na imani za kishirikina, kwani eti ndio mganga wao kawaambia hivyo ili wasifunge.
Mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe baada ya kuonekana kwa clip kadhaa ikiwemo clip ya game ya fainali ya UEFA Europa League kati ya Atletico Madrid dhidi ya Marseille, wachezaji wa Marseille kuanza mpira kwa kutoa nje, amesema kuwa Ajib amekosewa kwa hilo kuhusishwa na ushirikina.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Edo amepost clip ya Atletico dhidi ya Marseille na kuandika “Samahani Ajib wamekukosea sana…kumbe haikuwa uchawi bana….yalikuwa mambo ya kizungu yale… @hajismanara“
“Simba tumewaachia, sisi hatuna presha”-Kocha wa Yanga