Moja kati ya habari za kusisimua katika soka ni hii ya club ya Gulspor ya Uturuki kuamua kuwauza jumla ya wachezaji wake 18 kwenda vilabu vingine, halafu pesa iliyopatikana wakanunua mbuzi.
Gulspor imewauza jumla ya wachezaji 18 wa timu za vijana kwa lengo ya kiasi kilichopatikana, kuweza kununua mbuzi 10 kwa ajili ya kuanzisha biashara ya maziwa ya mbuzi ili kuiongezea club kipato.
Rais wa club Gulspor, Kenan Büyükleblebi inayoshiriki madaraja ya chini nchini Uturuki ameeleza kuwa mpango huo umekuja kutokana na club kushindwa kujimudu kiuchumi, hivyo biashara ya maziwa ya mbuzi itawasaidia kuongeza kipato cha gharama za uendeshaji wa timu.
Manji aibuka Yanga leo, asema ‘hakuna zawadi kubwa kama……….?’ (+video)