Usiku wa November 28 2018 club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa ili wakaribisha Liverpool ya England kucheza mchezo wao wa tano wa hatua ya makundi ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019.
PSG wakiwa nyumbani wameonesha faida ya kuwa nyumbani kwa kuifunga Liverpool kwa magoli 2-1, magoli ya PSG yakifungwa na Juan Bernat dakika ya 13 na Neymar dakika ya 37 kabla ya Liverpool kupata goli la kufutia machozi dakika ya 45 kupitia kwa James Milner.
Ushindi huo sasa unawafanya PSG kusubiri mchezo wa mwisho ili kuona kama watafuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 na kuuungana na timu za FC Barcelona, Atletico Madrid, Borussia Dortmund, FC Porto, Schalke 04, Man City, Man United, Juventus, AS Roma, Real Madrid na FC Bayern Munich waliyofuzu tayari.
EXCLUSIVE: Kauli ya Singida United kushindwa kulipa wachezaji, mbona wanasajili?