Klabu ya Dar Es Salaam Young Africans Jumamosi ya February 13 itaanza rasmi safari yake ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, kwa kucheza mchezo wake wa kwanza Mauritius dhidi ya wenyeji wao klabu ya Cercle De Joachim. Mkuu wa idara ya habari wa Yanga Jerry Muro ameeleza taarifa nzima ya Yanga kuelekea Mauritius.
- Yanga itaondoka Dar Es Salaam Alfajiri ya Jumtano ya February 10 na kuanza safari yake ya kuelekea Mauritius, ikiwa na list ya wachezaji 21, kasoro wachezaji Matteo Anthony hatokwenda kwa sababu anatajwa hayupo vizuri kwa mchezo huo, wakati Geofrey Mwashiuya na Benedict Tinoco hawatosafiri na timu wanashughulikia Passport zao Dar Es Salaam. Viongozi wa benchi la ufundi 7 na mkuu wa msafara atakuwa Ayoub Nyezi kutoka TFF.
- Mchezo utachezwa siku ya Jumamosi ya February 13 2016 saa 15:30 kwa saa za Mauritius katika mji wa Curepipe, waamuzi wa mchezo huo watatokea Madagascar na kamisaa akitokea Msumbiji.
- Yanga haitafikia hotelini kama ilivyozoeleka kwa mechi zake za kimataifa bali imekodi mahali maalum ambapo watakuwa watu wanaohusika na timu na wachezaji pekee. Baada ya mchezo huo Yanga watachelewa kurudi Dar Es Salaam ili wajiandae na mechi yao ya Ligi Kuu dhidi ya watani zao wa jadi Simba itakayochezwa February 20.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE